SIMBA YATAKA KUSEPA NA MAKOMBE YAO

MTENDAJI Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ameweka wazi kuwa Simba ipo imara na hesabu kubwa ni kutimiza malengo waliyojiwekea kutokana na wachezaji walionao kujituma.

Kwa sasa Simba inapambana kuweza kutetea taji lake ililotwaa msimu uliopita wakivutana kwa kasi na vinara wa ligi ambao ni Yanga wenye pointi 26 huku Simba wakiwa nafasi ya pili na pointi 21.

Barbara amesema kuwa wanazidi kufanya mambo mazuri kwa ajili ya timu na kwa sasa wanapambana kuweza kujenga uwanja.

“Tupo imara kwa namna ambavyo tunafanya hivyo mashabiki wasiwe na mashaka na sisi katika yale ambayo tunafanya, wachezaji wanajituma katika kutimiza majukumu yao.

“Imani yetu ni kwamba tutafanya vizuri kwenye ligi na kwenye Kombe la Shirikisho kwani haya nayo ni mashindano makubwa kimataifa kwa kuwa tupo kuiwakilisha nchi kimataifa, mashabiki wazidi kutuombea,” amesema Barbara