SIMBA WATAJA MIPANGO YAO

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa kazi kubwa ni kupata pointi tatu kwenye mechi ambazo wanacheza ikiwa ni mchezo dhidi ya Yanga.

Kariakoo Dabi inatarajiwa kuchezwa Aprili 20 2024 ambapo Yanga walimabingwa watetezi watawakaribisha Simba.

Simba imetoka kupata pointi moja dhidi ya Ihefu kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa Liti.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema wapo tayari kwa ajili ya mechi zinazofuata ndani ya ligi.

“Tunatambua kwamba tunamechi ngumu ambazo tunacheza hivyo tupo tayari kwa ajili ya kupata matokeo chanya mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.

“Wachezaji wapo tayari na wanatambua kwamba kila mchezo ni muhimu kwetu kupata ushindi, matokeo ambayo tunapata hayatufurahishi hivyo bado tunajipanga kupata matokeo,”.