Home Sports HIVI NDIVYO YANGA WANAICHUKULIA SIMBA

HIVI NDIVYO YANGA WANAICHUKULIA SIMBA

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa unawatazama wapizani wao Simba kwa utofauti kutokana na uimara walionao hivyo wanawaheshimu kuelekea mchezo wao wa Kariakoo Dabi.

Yanga vinara wa Ligi Kuu Bara wanatarajia kukutana na Simba kwenye mchezo wa Karikoo Dabi unaotarajiwa kuchezwa Aprili 20 2024.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua ukubwa wa mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba na wanawaheshimu.

Ipo wazi kwamba mwendo wa Simba haujawa imara na kwenye mchezo wao uliopita dhidi ya Ihefu waligawana pointi mojamoja kwa sare ya kufungana bao 1-1, Uwanja wa CCM Kirumba.

Yanga mchezo wao uliopita walipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Singida Fountain Gate wakisepa na pointi tatu mazima ndani ya dakika 90.

Kamwe amesema: “Tunatambua umuhimu wa mchezo wetu dhidi ya Simba na mchezo wetu ni mgumu huku tukiwatazama kwa umuhimu wapinzani wetu hivyo tunakwenda kupambana nao kwa umakini,”.

Previous articleSIMBA WATAJA MIPANGO YAO
Next articleBashiri na Meridianbet Jumatatu ya Leo