KIMATAIFA YANGA NI MUDATHIR YAHYA

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa kuelekea mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Mamelodi Sundowns itakuwa ni siku ya simu kuita kwa kuwa mchezo utakuwa kwenye miguu ya Mudathir Yahya.

Yahya chaguo la kwanza la Kocha Mkuu Miguel Gamondi amekuwa kwenye mwendelezo bora katika mechi za Ligi Kuu Bara ambapo mtindo wake wakushangilia pale anapofunga huonekana akiwa anaongea na simu hivi.
 
Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema: “Uongozi na benchi la ufundi wameazimia kwa pamoja kuwa mchezo wetu dhidi ya Mamelodi Sundowns, akabidhiwe kijana kutoka Kizimkazi, Mudathir Yahya. Slogani yetu kwenye mechi hii ‘SIMU ZIITE TUKUTANE KWA MKAPA’ Kazi ambayo tunayo kuanzia sasa hivi ni kupiga simu kwa watu wote tuwaambie tukutane kwa Mkapa,”

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90 za kuvuja jasho kwa wachezaji wa timu zote mbili kwenye anga la kimataifa.