MABAO SABA KUIKOSA TANZANIA PRISON LEO

WAKATI leo kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi kikitarajiwa kucheza mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela itakosa huduma ya nyota wake wanne ambao wamehusika kwenye jumla ya mabao saba.

Yanga yenye pointi 20 ipo nafasi ya kwanza na safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 12 na ukuta wake umeruhusu mabao mawili inakutana na Prisons iliyo nafasi ya 13 na pointi nane.

Nyota wake wanne ambao hawatakuwa sehemu ya kikosi ni pamoja na Yacouba Songne mwenye pasi mbili za mabao huyu anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima kwa kuwa aliumia mguu kwenye mchezo dhidi ya Ruvu Shooting.

Pia Mayele naye alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Simba yeye ametupia mabao matatu na pasi moja ya bao na beki wao kitasa Kibwana Shomari mwenye pasi moja ya bao naye hatakuwa sehemu ya kikosi kwa kuwa aliumia goti.

Kwa ujumla wake nyota hao watatu wamehusika kwenye mabao saba kati ya 12 mbali na hao pia yupo Yusuf Athuman ambaye yeye ni mshambuliaji.

Wengine ambao wanatarajiwa kuukosa mchezo huo ni pamoja na Mapinduzi Balama na Dickson Ambundo.