MZIZIMA Dabi imeacha mengi ambapo Simba ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na matajiri wa Dar ambao walianza kufunga dakika ya 14 kupitia kwa Prince Dube ambaye amekuwa na zali la kuwatungua Simba.Chama alionyesha ubora wake mwishoni alipofunga bao kwa pigo huru.