KAIMU Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Yanga, Senzo Mbatha Mazingisa amesema kuwa kila siku
anazidi kufurahishwa na utendaji kazi na juhudi kubwa inayoonyeshwa na wachezaji wa timu hiyo kuwa ni kazikubwa inayofanywa na benchi la ufundi chini ya kocha Nabi.
Katika msimu huu, Yanga ilianza kwa kutwaa ubingwa wa Ngao ya Jamii na hadi sasa Yanga imekaa kileleni katika msimamo wa ligi Kuu kwa pointi tisa katika michezo yote mitatu iliyocheza.
Senzo amesema kuwa shukrani zake zote ziende kwa Nabi kwani amejitahidi kukibadilisha kikosi cha timu hiyo tofauti na siku za mwanzoni Yanga ilivyokuwa inapoteza
Hadi sasa Yanga ilipofikia shukrani zangu za dhati ni kwa kocha Nabi na bechi zima la ufundi kwa sababu
ukiangalia kuanzia mwanzo wa msimu huu hadi sasa unaweza kuona kuna tofauti kubwa sana.
“Katika kila mchezo unaona kabisa wachezaji wanazidi kuimarika, wanafanya vizuri, hii inaonyesha ni kiasi gani kocha Nabi anafanya kazi kubwa hadi hapa tulipofikia.
“Msimu huu unaonekana kuwa mgumu sana lakini nina imani kuwa chini ya kocha Nabi mambo yatakuwa kama tulivyopanga kwa sababu hata kikosi chake anakipangilia vizuri, hilo linamfanya aonekane ni kocha mwenye uelewa na kazi yake,” alisema kiongozi huyo.