Home Sports SIMBA YAFUNGUKIA KASI YA YANGA

SIMBA YAFUNGUKIA KASI YA YANGA

MWENYEKITI wa Simba, Murtaza Mangungu, amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kwa kuwaambia wasiogope kasi ya wapinzani wao Yanga huku akiahidi kuubakisha ubingwa wa Ligi Kuu Bara Msimbazi.

 

Kauli hiyo ameitoa baada ya kuiona Yanga ikiwa kileleni ikiwa na pointi tisa, ikishinda michezo yake
mitatu ya ligi katika msimu 
huu.


Simba yenyewe imecheza 
michezo miwili kati ya hiyo wametoka suluhu na Biashara United huku ikiwafunga
Dodoma Jiji bao 1-0, 
lililofungwa na Mnyarwanda, Meddie Kagere.


“Mechi tatu haziwezi 
kuwapa ubingwa au kututoa kwenye mbio za ubingwa. Ligi ni mbio ndefu na sisi Simba ubingwa wetu uko palepale.


“Wanasimba waondoe hofu, 
tupo vizuri kama viongozi katika utendaji, pia benchi la ufundi linaloendelea kufanya maandalizi ya kikosi chao,” alisema Mangungu.

Previous articleSENZO AKUBALI UWEZO WA NABI
Next articleOLE ANAONA MAMBO MEUSI