>

HAJI MANARA AFUNGUKIA ISHU YA TUZO

OFISA Habari wa Yanga, Haji Manara amefunguka baada ya kubwagwa kwenye tuzo za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) msimu wa 2020/21, kipengele cha Muhamasishaji Bora.

Tuzo hiyo ilikwenda kwa shabiki kindakindaki wa Taifa Stars, Nick Renold maarufu kama Bongo Zozo, ambaye aliwashinda Manara na Masau Bwire wa kKlabu ya Ruvu Shooting.

Manara ambaye alikuwa akiwania tuzo hiyo kwa kushindwanishwa na Ofisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire pamoja na mshindi Bongo Zozo amesema kuwa mshindi amestahili.

Bongo Zozo  yeye aliweka wazi kwamba hakustahili kutangazwa kuwa mshindi na iwapo yeye ndiyo angekuwa anatoa tuzo hiyo, angempa Manara.

Bongo Zozo anaamini Manara alistahili tuzo hiyo kwa kazi kubwa ya kuwahamasisha Mashabiki aliyoifanya kwa timu ya Taifa Stars na alipokua Simba SC kabla ya kuhamia Yanga.

Manara alipokutana na Bongo Zozo alimpa pongezi zake kwa kutwaa tuzo hiyo na kumwambia kwamba amestahili kupewa hiyo tuzo.

“Wewe umestahili kupokea tuzo na haina tatizo, hongera katika hilo wewe ni rafiki yangu na jirani yangu pia kazi lazima iendelee,”.