>

YANGA YAWATULIZA MEDEAMA KWA MKAPA NA KUKOMBA POINTI

YANGA wameonyesha ubabe wao mbele ya Medeama katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika uliochezwa Uwanja wa Mkapa wakiwatuliza wapinzani wao hao na kukomba pointi tatu mazima.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Yanga 3-0 Medeama FC ikiwa ni mchezo wa nne Kwa Yanga.

Mabao ya Pacome Zouzoua dakika ya 33, Bakari Mwamnyeto dakika ya 60 na kamba ya tatu ni Mudathir Yahya dakika ya 80.

Yanga inafikisha pointi tano ikiwa nafasi ya pili kundi D huku Medeama wakiwa nafasi ya tatu na CE Belouizdad nafasi ya nne wakiwa na pointi nne.

Vinara ni Al Ahly wenye pointi tano tofauti katika mabao ya kufungwa na kufunga.