SABABU ZA BARBRA KUPIGWA STOP KUITAZAMA SIMBA V YANGA HIZI HAPA

WAKATI jana Desemba 11, Uwanja wa Mkapa mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba v Yanga ukipigwa jukwaani hakuwepo kabisa Mtendaji Mkuu wa Simba,Barbara Gonzalez ambaye inatajwa kwamba alizuiwa kuweza kuutazama mchezo huo.

Ikumbukwe kwamba Barbara alitumia mitandao yake ya kijamii kuzungumza na mashabiki wa Simba kwa kuwambia kwamba alifika Uwanja wa Mkapa na familia yake akiwa na kila kitu kinachomruhusu kuweza kuingia uwanjani.

Barbara amesema:”Asante sana Tanzania Premier League Board, (TPLB wasimamizi wakuu wa Ligi Kuu Bara,) kwa kunizuia kuingia kwenye mechi na familia yangu. God Bless Tanzania, (Mungu ibariki Tanzania),God Bless Simba, (Mungu ibariki Simba), aliandika kiongozi huyo.

Baada ya taarifa hiyo, Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) lilitoa taarifa na kusema:”Tumesikitishwa na vitendo vya vurugu vilivyofanywa na baadhi ya viongozi wa Simba kwenye eneo la kuingilia Jukwaa la Watu Maalum, (VVIP) Uwanja wa Benjamin Mkapa kabla ya mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Simba SC na Yanga SC.

“Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbra Gonzalez alifika katika eneo hilo akiwa na watoto watatu ambao hawaruhusiwi kuingia katika eneo hilo la VVIP.

“Watoto hao ambao waliongozana naye walikuwa na kadi za watu wengine walioalikwa kinyume na utaratibu unavyotakiwa.

“Barbara ambaye yeye aliruhusiwa kuingia alianza kutoa lugha isiyofaa kwa Ofisa wa TFF huku akirekodi video na baadaye kutupa kadi na kuondoka.

“Katika hatua nyingine viongozi wa Simba walifanya vurugu kwenye eneo la kuingilia baada ya kutaka kulazimisha mmoja wa viongozi kuingia bila ya kadi ya mwaliko.

“Tukio hilo limeripotiwa kwenye mamlaka husika zinazosimamia mchezo,”