WAKALI WA 5 G KWENYE KAZI NYINGINE LEO TANGA

MABINGWA mara 29 wa Ligi Kuu Bara Yànga leo wanakibarua cha kusaka pointi tatu dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Chini ya Miguel Gamondi, Novemba 5 2023 walishuhudia ubao wa Uwanja wa Mkapa ukisoma Simba 1-5 Yànga.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa kuna ushindani mkubwa kwenye ligi na mechi ambazo wanacheza zimeongozana hivyo ugumu upo.

Yanga inaongoza kwenye safu namba moja kali ya utupiaji ikiwa na mabao 25 huku wakali wawili Aziz KI na Maxi Nzengeli wakiwa wote wametupia mabao sabasaba.

“Ni mchezo mgumu kwetu kulingana na namna ligi ilivyo ukizingatia kwamba tumetoka kucheza mchezo hivi karibuni.

“Ambacho tunakifanya ni kuendelea kujitahidi kufanyia kazi makosa ili kupata matokeo kwa kuwa hilo ni jambo la muhimu kwetu,”.

Miongoni mwa nyota ambao wapo Tanga ni pamoja na Pacome Zouzoua mwenye mabao manne ndani ya ligi na pasi moja ya bao.