NYOTA SIMBA ASHUSHA PRESHA, YUPO FITI KWA KAZI

KIUNGO wa Simba raia wa Ivory Coast, Aubin Kramo amerejea nchini akitokea nyumbani kwao kwa ajili ya matibabu na sasa anaendelea vizuri akisubiria taratibu za kurejea uwanjani kuipambania timu yake.

Kiungo huyo wiki moja iliyopita aliomba ruhusa kwa uongozi wa Simba ili arejee nyumbani kwao kwa ajili ya kwenda kujiuguza majeraha yake ya goti ambayo yanamtesa mara kwa mara.

Daktari wa wa timu hiyo, Edwin Kagabo alisema kiungo huyo anaendelea vizuri na matibabu ya goti na hivi sasa anasubiria taratibu za kujua lini atarejea uwanjani tena.

Kagabo amesema Kramo amesharudi baada ya kwenda, Ivory Coast kwa uchunguzi zaidi, lakini bado hajaruhusiwa kuanza mazoezi na wachezaji wenzake kikosini.

“Kwa sasa siwezi kuweka wazi ni lini atarudi kwa sababu kuna awamu ambazo sisi kama madaktari tumempa na tunaendelea kumfanyia uchunguzi hatua kwa hatua.

“Lakini kikubwa mashabiki wa Simba watambue jeraha lake sio la kumuweka nje ya uwanja muda mefu kwa kuwa sio kubwa, watarajie kumuona akirejea mapema kuipambania timu yake.

“Sisi madaktari wa timu, tunaendelea kupambana ili kuhakikisha anarudi haraka iwezekanavyo kwani mashabiki wengi wana shauku kubwa ya kumuona akikitumikia kikosi hicho kutokana na ubora aliokuwa nao,” amesema Kagabo.