Home Sports YANGA YAFUTA MATOKEO YA KIMATAIFA, KAZI AZAM COMPLEX

YANGA YAFUTA MATOKEO YA KIMATAIFA, KAZI AZAM COMPLEX

BENCHI la ufundi la Yanga limeweka wazi kuwa ushindi wa mabao 0-2 waliopata dhidi ya Al Merrikh, Waarabu wa Sudan wameyafuta yote na akili zao ni kupata ushindi kàtika mchezo wa leo.

Chini ya Miguel Gamondi kikosi cha Yanga kinatarajiwa kutupa kete yake ya pili kàtika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa leo Uwanja wa Azam Complex.

 Gamondi amesema kuwa baada ya mchezo uliopita ugenini na kupata matokeo yote walisahau na kuanza kujipanga upya Kwa mchezo wa nyumbani.

“Tumesahau matokeo yaliyopita ugenini licha ya kuwa tulipata ushindi ambacho tunakifanyia kazi kwa sasa ni kuhakikisha tunapata matokeo chanya katika mchezo wetu ambao tutakuwa uwanjani.

“Maandalizi yalikuwa kwa muda tulipomaliza mchezo uliopita na tunatambua haitakuwa kazi nyepesi kwetu. Kazi kubwa ipo katika kutafuta matokeo mengine katika mchezo wetu muhimu.

“Katika dakika 45 za mwanzo ugenini tulifanya makosa mengi Hilo tuliliona na tulifanyia kazi kwa umakini katika eneo la mazoezi.

“Kuhusu wachezaji watakaokosekana katika mchezo wetu sitaweza kuwataja kwani nitakuwa ninawapa mbinu wapinzani wetu kuelekea mchezo huo,” amesema Gamondi.

Miongoni mwa wachezaji wa Yanga ambao walikuwa kwenye mazoezi ya mwisho ni Sure Boy, Aziz KI, Kennedy Musonda, Dickson Job.

Osama Nabieh Kocha Mkuu wa Al Merrikh amesema kuwa wanahitaji matokeo katika mchezo dhidi ya Yanga.

“Tumejipanga kupata matokeo kwenye mchezo wetu dhidi ya Yanga licha ya kwamba wao wanafaida ya kupata ushindi kwenye mchezo tuliokutana mwanzo.

“Katika mpira chochote kinawezekana hivyo ni Jambo la kusubiri baada ya dakika 90 kile ambacho tutakipata na tunatambua wapinzani wetu watakuwa nyumbani,” alisema.

Previous articleKIMATAIFA MALIZIENI MKIA KWA UMAKINI
Next articleNYOTA SIMBA ASHUSHA PRESHA, YUPO FITI KWA KAZI