Home Sports KIMATAIFA MALIZIENI MKIA KWA UMAKINI

KIMATAIFA MALIZIENI MKIA KWA UMAKINI

WIKI ya kutambua mbivu na mbichi kwenye anga la kimataifa hii hapa imefika ambapo kila mmoja atavuna kile ambacho atakipanda ndani ya dakika 90.

Yale majigambo ya nje ya uwanja muda wake unakwenda kugota mwisho kwani ipo wazi kuwa hakuna marefu yasiyokuwa nan cha.

Muda huu uliobaki kwa wawakilishi wetu kimataifa ni kuchanga karata kwa umakini. Kupata matokeo chanya kwenye mechi hizi za marudiano ni mwanzo wa mwendelezo hatua nyingine.

Hatua moja kwenye anga la kimataifa inapigwa taratibu, umakini na kujitoa kwa wachezaji utaleta majibu mazuri. Presha kubwa kutoka kwa mashabiki isiwape unyonge wachezaji bali wacheze kwa kujiamini.

Watakaopewa majukumu ya kuanza kikosi cha kwanza ni muda kuonyesha kweli. Kazi ikiwa nzuri ni faida kwa timu na mchezaji binafsi.

Mchezaji ataongeza thamani kwenye soko na timu itaongeza thamani ya rekodi na kuzidi kutambulika mbali zaidi. Weka mbali hilo soka la Tanzania litazidi kuvuka anga kimataifa kutokana na ubora wa wachezaji kwenye kutimiza majukumu.

Muda ni sasa na inawezekana. Sio Yanga ambao walipata ushindi wala Singida Fountain Gate haijagota mwisho mpaka igote kabisa.

Simba wao waliambulia sare kazi ipo kwenye kusaka ushindi nyumbani. Hakuna namna kama walipata mabao ugenini basi wana nafasi ya kupata mabao nyumbani.

Lakini hakuna timu yenye uhakika na matokeo kwa kuwa mpira unadunda muhimu umakini ndani ya dakika 90.

 

Previous articleWAZIRI WA MICHEZO ATOA NENO KWA YANGA KIMATAIFA NA UJUMBE WA MAMA
Next articleYANGA YAFUTA MATOKEO YA KIMATAIFA, KAZI AZAM COMPLEX