Home Sports WAZIRI WA MICHEZO ATOA NENO KWA YANGA KIMATAIFA NA UJUMBE WA MAMA

WAZIRI WA MICHEZO ATOA NENO KWA YANGA KIMATAIFA NA UJUMBE WA MAMA

WAZIRI wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Damas Ndumbaro amesema kuwa Serikali ipo pamoja na Yanga kuhakisha inapata ushindi kwenye mchezo wa kimataifa dhidi ya Al Merrikh.

Leo inatarajiwa kuwa burudani ya Key Dey Septemba 30 ambapo Yanga inatarajiwa kutupa kete yake dhidi ya Al Merrekh.

Huu ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Azam Complex.

Katika kuwapa nguvu wachezaji wa Yanga kuendeleza pale walipoishia kwa kupata ushindi ugenini wa mabao 0-2 Ndumbaro alipata muda wa kuwatembelea wachezaji kambini Avic Town.

Mchezo wa leo umepewa jina la Key Dey ukimtambulisha Aziz KI amaye huvaa jezi namba 10 mgongoni.

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo ili kutinga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.

Ndumbaro amesema “Rais wetu Samia Suluhu Hassan anawapongeza sana kwa hatua mliyofika na anawatakia kila la kheri kwenye mchezo wenu dhidi ya Al-Merrikh, Serikali iko pamoja nanyi kuhakikisha mnaendelea kuiwakilisha vyema nchi yetu kwenye anga za Kimataifa”

Previous articleUSITUPE NGUVU ZAKO BURE KUONYESHA TFF YA KARIA HAIJALETA AFCON TANZANIA
Next articleKIMATAIFA MALIZIENI MKIA KWA UMAKINI