KIUNGO wa Simba, Saidi Ntibanzokiza ‘Saido’ ameandika rekodi yake kimataifa kwa kuwa nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano kwenye hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa upande wa Simba, dakika mbili akiwa uwanjani.
Simba ilikuwa na kibarua cha kusaka ushindi kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos ambapo Ntibanzokiza alianzia benchi.
Alipopewa nafasi ya kuingia dakika ya 60 akichukua mikoba ya Willy Onana dakika ya 62 alicheza faulo iliyopelekea mwamuzi kumuonyesha kadi ya njano ikiwa ni ya kwanza kwake na Simba kiujumla katika anga la kimataifa msimu wa 2023/24.
Mbali na kuwa nyota wa kwanza kuonyeshwa kadi ya njano Ntibanzokiza alikosa nafasi ya dhahabu kupachika bao ilikuwa dakika ya 65.
Ni shuhuda ubao wa Levy Mwanawasa, Zambia ukisoma Power Dynamo 2-2 Simba huku mabao yote ya Simba yakifungwa na Clatous Chama.
Kete ya pili inatarajiwa kuchezwa Oktoba Mosi, Uwanja wa Azam Complex ambapo mshindi wa jumla atakata tiketi ya kusonga hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.