MWAMBA HUYU HAPA NDANI YA YANGA ANASUKWA UPYA

NYOTA wa Yanga, Clement Mzize anasukwa upya ili kuongeza makali yake kwenye kufunga mabao kwenye mechi za kitaifa na kimataifa.

Mzize ambaye ni mzawa ni chaguo la kwanza chini ya Kocha Mkuu, Miguel Gamondi amekuwa akipewa program maalumu kwa ajili ya kuimarika zaidi awapo uwanjani.

 Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe amesema kuwa wachezaji wote wanapewa mbinu na benchi la ufundi ili kuwa imara kwenye mechi zote za ushindani.

“Tunaye Mzize ambaye yeye ni mshambuliaji mwenye uwezo mkubwa hilo linazidi kudhihirika taratiu, bahati mbaya kila tunaposema vitu wengi hutupuuzia lakini huo ni ukweli wachezaji wanapewa mbinu kuwa imara zaidi.

“Ushirikiano uliopo kwenye benchi la ufundi pamoja na nguvu za wachezaji kutimiza majukumu yao linaongeza kasi ya kufikia mafanikio ambayo tunahitaji,” amesema Kamwe.

Nyota huyo kibindoni ametupia mabao mawili na yote ni Ligi ya Mabingwa Afrika ilikuwa dhidi ya ASAS FC dakika ya 70 na Al Merreikh ilikuwa dakika ya 78.

Uwezo wake wa kuwa na hatari ni ndani ya eneo la 18 ambapo aliwatungua ASAS FC kwa pigo la kichwa na Al Merreikh ilikuwa ni kwa mguu wake kulia.