Home Sports CLEMENT MZIZE ANA BALAA HUYO

CLEMENT MZIZE ANA BALAA HUYO

NYOTA wa Yanga, Clement Mzize ni habari nyingine Bongo kwa upande wa mastaa wanaocheza ndani ya Yanga na Simba kwa kuwa mzawa aliyepachika bao kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, vigogo wote walipokuwa kazini.

Ikumbukwe kwamba Septemba 16, Yanga ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Al Merrikh, Rwanda na Simba ilikuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo dhidi ya Power Dynamos, Zambia.

Mzize ambaye ni mzawa yeye alipachika bao dhidi ya Al Merreikh waliposhinda kwa mabao 0-2 huku lile lingine likifungwa na Kennedy Musonda raia wa Zambia.

Kwa upande wa Simba walishuhudia ubao ukisoma Power Dynamos 2-2 Simba ambapo mabao yote ya Simba yalifungwa na Clatous Chama raia wa Zambia.

Hivyo mabao ya Septemba 16 kwa wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambayo ni manne, matatu yalifungwa na nyota kutoka Zambia huku moja likpachikwa kimiani na mzawa Mzize ambaye ni habari nyingine kwa sasa Bongo kutokana na kupewa nafasi kuanza kuoyesha makeke yake.

Previous articleSAIDO AWEKA REKODI YAKE ANGA ZA KIMATAIFA
Next articleAFYA YA WACHEZAJI NI MUHIMU, WACHEZAJI LINDANENI