SIMBA YATUPWA NJE LIGI YA MABINGWA AFRIKA

 

TIMU ya Simba imetolewa rasmi kwenye michuano ya Ligi Mabingwa Afrika baada ya kufungwa Jwaneng Galaxy kwa mabao 3-1, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa.

 

Simba ambayo ilianza vema kipindi cha kwanza ilienda mapunziko ikiwa mbele kwa bao 1-0 goli la Larry Bwalya, lakini Galaxy waligeuza kibao kupachika magoli 3.

 

Matokeo ya Jumla ni 3-3 lakini Simba imetolewa kwa baada ya Galaxy kuwa na magoli mengi ya ugenini sasa Simba itacheza kwenye michuano ya kombe la shirikisho.