NGOMA SITA BORA KAZIKAZI, RATIBA YAO HII HAPA

KILE ambacho wanazidi kukionyesha Arsenal kwenye Premier League pengine wengi hawakutarajia kwamba hadi sasa wangekuwa wanakalia kileleni mwa msimamo tena dhidi ya klabu ambazo zinaonekana zilizoeleka kwenye nafasi hiyo Manchester City na Liverpool.

Arsenal kwa sasa ndio wako kileleni kwa tofuti ya alama tano dhidi ya wanaowafuatia ambao ni Man City na 11 dhidi ya Man United.

Haya ni sehemu ya matunda ya usajili mzuri ambao waliufanya kwenye majira ya joto kwa kuingiza silaha muhimu kulingana na mahitaji ya Kocha Mikel Arteta.

Sio Arsenal pekee walioingia sokoni na kununua bali ni klabu zote za ‘Big Six’ zinazojumuisha Chelsea, Man United, Man City, Liverpool, Spurs na Arsenal.

Hadi sasa ukiangalia msimamo, Arsenal ndio wako kileleni na pointi zao 50 ambazo wamezipata baada ya kucheza mechi 19, wakishinda 16, sare mbili na kupoteza mara moja. Wamefunga mabao 45 na wao wameruhusu mabao 16.

Wanaofuatia ni Man City wana pointi 45 baada ya kucheza mecho 20. Wageni Newcastle wana alama 39 baada ya mechi 20, hii ndio timu iliyoruhusu mabao machache zaidi kwenye ligi nzima. Man United nafasi ya nne pointi 39 wakicheza mechi 20 halafu Spurs wa tano na alama zao 36, nje ya hapo kuna wakubwa wawili big six ambao wako nje ya tano bora hadi sasa.

Liverpool anashika nafasi ya tisa na alama zake 29 baada ya kucheza mechi 19 huku Chelsea akiwa wa 10 na pointi zake 29 yeye amecheza mechi 20.

Hapa nimekuandalia ratiba ya klabu sita kubwa ‘big six’ pale Premier kwa mwezi huu wa pili, unadhani watatoboa kwa namna ratiba yao ilivyo? Arsenal ataendelea kushikiria usukani, je City ya Erling Haaland itafanikiwa kupunguza ‘gepu’ la pointi dhidi yao? Tusubiri.

Ratiba yao iko hivi; A inamaanisha ugenini na H inamaanisha nyumbani.

RATIBA YA ARSENAL

Februari 4—Everton vs Arsenal (A)

Februari 11—Arsenal vs Brentford (H)

Februari 15—Arsenal v Man City (H)

Februari 18—Aston Villa vs Arsenal (A)

Februari 25— Leicester vs Arsenal (A)

RATIBA YA MANCHESTER CITY

Februari 5—Tottenham vs Man City (A)

Februari 12—Man City vs Aston Villa (H)

Februari 15—Arsenal v Man City (H)

Februari 18—Nottingham vs Man City (A)

Februari 25—Bournemouth vs Man City (A)