JANUARI bado inaendelea na maneno kuhusu huyu mwamba ndani ya Manchester City ni balaa.
Kwa kutupia dani ya Premier League ni mkali wa kutupia kwenye ligi zote duniani zenye ushindani mkubwa.
Mabao yake 25 yamewaacha mabeki wa Premier League wakiwa na hofu akivunjavunja rekodi za wababe wengi ndani ya ligi hiyo pendwa.
Amevuka idadi ya mabao ambayo Mohamed Salah na Son Heung-min walifunga na kushinda kiatu cha dhahabu msimu uliopita.
Sahau idadi yake kubwa ya mabao kwenye kutupia na hana chaguo akifika kwenye eneo la lango zaidi ya kutupia tu.