MESSI AFUNGA BAO LAKE LA KWANZA KWENYE LIGI

MSHAMBULIAJI wa kikosi cha PSG, Lionel Messi ameingia kwenye rekodi ya wale  waliopata nafasi ya kufunga kwenye Ligi Kuu Ufaransa.

Messi alifunga bao moja kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Nates na PSG iliweza kushinda kwa mabao 3-1 ikiwa nyumbani.

Mshambuliaji huyo alijiunga na timu hiyo akitokea Klabu ya Barcelona na mwanzo wa msimu wa 2021/22 alikuwa bado hajaweza kufunga.

Mabao mengine yalifungwa na Kylian Mbappe na Dennis Appiah alijifunga.