ARSENAL YAPIGWA 4G

KLABU ya Liverpool imeishushia kichapo cha mabao 4-0 Arsenal katika mchezo wa Ligi Kuu uliochezwa Uwanja wa Anfield.

Mabao ya Sadio Mane dakika ya 39,Dogo Jota dakika ya 52,Mohamed Salah dakika ya 73 na Takumu Minamino dakika ya 77 yalitosha kuituliza Arsenal.

Ni jumla ya mashuti 19 ambayo Liverpool ilipiga huku 9 yakilenga lango katika mchezo huo na Arsenal walipiga mashuti matano pekee na matatu yalilenga lango.

Ushindi huo unaifanya Liverpool kufikisha pointi 25 nafasi ya pili huku Arsenal ikiwa nafasi ya tano na pointi 20 kibindoni.