MANCHESTER UNITED WANYOOSHWA UGENINI

DAVID De Gea kipa namba moja wa Manchester United amesema kuwa wapo kwenye wakati mgumu kwa sasa kutokana na matokeo ambayo wanayapata ila wanawashukuru mashabiki kwa namna ambavyo wanakuwa nao.

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Watford 4-1 Manchester United.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Vicarage Road licha ya uwepo wa Cristiano Ronaldo ndani ya United kichapo hakikukwepeka.

Mabao ya Joshua King dk 28,Ismaila Sarr dk 44,Joao Pedro dk 90+2 na Emmanuel dk 90+6 yaliinyoosha Manchester United iliyopata bao moja kupitia kwa Donny van de Beek dakika ya 50.

Beki wao Harry Maguire alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 69 na kuwafanya United kumaliza dakika 90 wakiwa pungufu katika mchezo huo.

United inabaki na pointi 17 ikiwa nafasi ya 7 huku Watford ikifikisha pointi 13 ipo nafasi ya 16 katika msimamo wa Ligi Kuu England.