Home Sports MALENGO YA SIMBA NI KUTWAA MATAJI

MALENGO YA SIMBA NI KUTWAA MATAJI

MIRTAZA Mangungu, Mwenyekiti wa Klabu ya Simba amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kuhakikisha kwamba wanashinda mataji.

Simba ni mabingwa watetezi wa ligi wakiwa nafasi ya pili na pointi 14 huku Yanga wakiwa ni vinara wa ligi na wana pointi 16.

Maneno hayo ameyasema katika mkutano mkuu wa Wanachama wa Simba ambao unafanyika leo Novemba 21 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mikitano wa Julius Nyerere.

“Kama ilivyo nalengo ya Simba ni kuhakikisja tunashinda mataji. Naomba tuendelee kushirikiana ili tufanikishe jambo hili,”.

Kabla ya Wanachama kuingia kwenye mkutano wa leo walikuwa wanahakikiwa kadi zao pamoja na suala la kulipia ada ya uanachama.

Previous articleMANCHESTER UNITED WANYOOSHWA UGENINI
Next articleKMC V AZAM FC KUKIWASHA LEO