>

KIUNGO YANGA APEWA TUZO YA MCHEZAJI BORA

KIUNGO Khalid Aucho wa Klabu ya Yanga, amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka kutoka nchini Uganda.

Aucho mwenye miaka 29 amefanikiwa kushinda tuzo hiyo baada ya kuwashinda wapinzani wake katika kinyang’anyiro hicho.

Kiungo huyo amefanikiwa kuwashinda kipa wa Mamelodi Sundowns, Dennis Masinde Onyango mwenye miaka 37 na mshambuliaji wa Vipers Yunus Sentamu mwenye miaka 28.

Aucho ni chaguo la kwanza ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi