Makonda Awasili Qatar Kuipa Hamasa Serengeti Boys Kabla ya Mchezo Dhidi ya Ireland

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, amewasili jijini Doha, Qatar, kwa ziara ya kikazi inayolenga kuongeza hamasa kwa timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys, inayoshiriki michuano ya Kombe la Dunia nchini humo.

Makonda amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini Qatar, Habibu Awesi Mohamed, pamoja na viongozi wengine wa Serikali waliopo nchini humo kwa mafunzo maalumu.

Katika ziara hiyo, Waziri Makonda anatarajiwa kukutana na kutoa hamasa kwa vijana wa Serengeti Boys wanaoiwakilisha Tanzania katika mashindano hayo ya kimataifa.

Aidha, Waziri huyo anatarajiwa kushuhudia mchezo muhimu kati ya Serengeti Boys na timu ya taifa ya vijana ya Ireland, unaotarajiwa kuchezwa leo, Novemba 27, 2026, nchini Qatar.

Ujio wa Makonda unalenga kuonesha mshikamano na kuiunga mkono timu hiyo katika jitihada zake za kuipeperusha vyema bendera ya Tanzania kwenye michuano hiyo ya dunia.