Pocchettino Arejea EPL, Safari Yake na Man United Yaanza Kwa Presha

Macho yote sasa pale Old Trafford yapo kwa kocha mpya wa United Pochettino ambaye amepewa kazi ya kuinoa timu. Mechi mbili za kwanza ataondoka na ushindi?

Michael Carrick ameiacha Man United ikiwa nafasi ya 18 kwenye msimamo wa ligi, yaani nafasi ya 3 kutoka chini kwenye kushuka daraja baada ya kucheza mechi 10 hadi sasa huku mara ya mwisho kushinda kwenye ligi ilikuwa ni mwezi Agosti wakiwa wameshinda mechi moja pekee.

Wengi wanasema kuwa tatizo la United si matokeo pekee, bali pia kushindwa kupata mwendelezo mzuri wa mchezo. Katika mechi zake za hivi karibuni, ilipoteza dhidi ya Bournemouth kwa mabao 3-0 na Chelsea kwa mabao 2-0, kabla ya kutoka sare ya mabao 4-4 dhidi ya Aston Villa. Licha ya uwezo wa Bruno Fernandes na Bryan Mbeumo kuchangia mabao, timu imekuwa ikishindwa kulinda matokeo na kuzuia wapinzani kupata nafasi za kufunga. Jisajili hapa.

Nafasi ya ushindi ipo kwenye michezo ya Kasino ya Mtandaoni kama vile, Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli na mingine kibao. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Kwenye michuano ya ligi ya Mabingwa yaani Uefa pia bado hali ni mbaya ambapo United imerejea kushiriki michuano hiyo baada ya misimu miwili, lakini bado mwenendo wao hauridhishi  kwani mpaka sasa inashika nafasi ya 17 wakiwa na pointi 6 pekee hadi sasa kwenye mechi 4 ambazo wamecheza.

Mchezo unaofuata watakipiga dhidi ya Sporting CP utakuwa mtihani muhimu kwa kikosi hicho, hasa ikizingatiwa kuwa kinahitaji kuboresha matokeo ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele.

Kutokana na mwenendo huo, klabu iliamua kumuondoa Michael Carrick kwenye nafasi ya kocha mkuu Novemba 12. Carrick alikuwa amepewa nafasi hiyo baada ya kuondoka kwa Ruben Amorim, na aliwahi kuiongoza United kumaliza nafasi ya tatu kwenye EPL msimu uliopita na kufuzu Champions League. Hata hivyo, mwanzo mbaya wa msimu mpya, ukiwemo mfululizo wa mechi bila ushindi, ulifanya uongozi wa klabu kuchukua uamuzi wa kubadilisha benchi la ufundi.

Mauricio Pochettino amepewa mkataba utakaodumu hadi mwaka 2029. Kocha huyo an uzoefu mkubwa na ligi hiyo ambapo tayari ameonoa vilabu kama Tottenham Spurs pamoja na Chelsea kabla ya kwenda kuinoa timu ya Taifa ya Marekani.

Kocha huyo ataanza mtihani wake wa kwanza na mechi dhidi ya Liverpool kule Anfield, moja ya mechi ngumu sana kwa upande wa Mashetani Wekundu na hapo baadae atasafiri kwenda kule Ureno kusaka ushindi dhidi ya Sporting CP. Je kocha huyo ataanza vipi mechi hizo?. Beti sasa.

Mashabiki mbalimbali wanasema kuwa klabu hiyo kwa ujumla inahitaji zaidi ya kubadilisha kocha inahitaji kurekebisha mfumo wa uchezaji, kuongeza uimara wa ulinzi na kurejesha ushindani. Pochettino ana kazi kubwa ya kuifanya timu iondoke kwenye eneo la hatari la kushuka daraja na kuanza kupigania nafasi za juu, huku akihakikisha safari yake ya Champions League haiishii mapema.