Kampuni ya ubashiri ya Meridianbet imeendelea kutekeleza dhamira yake ya kurudisha kwa jamii kupitia mpango wake wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR), kwa kukabidhi vifaa vya usafi wa mazingira kwa wajasiriamali katika maeneo mbalimbali ya mitaa ya Upanga, jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo limefanyika kwa kushirikiana na wafanyabiashara pamoja na wajasiriamali, likiwa na lengo la kuhamasisha usafi wa mazingira, utunzaji wa taka na kuimarisha mazingira bora na salama kwa wafanyabiashara pamoja na wananchi wanaowahudumia kila siku.
Kupitia msaada huo, Meridianbet inalenga kuwasaidia wajasiriamali kuwa na maeneo safi ya kufanyia biashara zao kwa kuweka taka katika sehemu maalumu badala ya kuzitupa ovyo, hatua inayoweza kuchangia kupunguza uchafuzi wa mazingira na kuboresha afya ya jamii.

Vilevile, meridianbet wana michezo mingi ya kasino mtandaoni na mechi za kimataifa za kubashiri zenye ushindani mkubwa wa odds. Jiunge leo kwa kutembelea tovuti ya MERIDIANBET au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Akizungumzia msaada huo, Nancy Ingram kutoka Meridianbet amesisitiza umuhimu wa kushirikiana na wananchi wa maeneo husika pamoja na makundi mbalimbali ya kijamii katika kutatua changamoto zinazowakabili wananchi na kuendeleza mazingira bora kwa wote.
Kwa upande wake, ushirikiano na wajasiriamali hao unaonesha umuhimu wa kuunganisha nguvu za sekta binafsi na watumiaji wa maeneo husika katika kuhamasisha maendeleo ya jamii na utekelezaji wa mipango yenye manufaa kwa wananchi.

Meridianbet inaamini kuwa usafi wa mazingira ni jukumu la kila mmoja. Hivyo, kampuni inatoa wito kwa wajasiriamali wote na wananchi kwa ujumla kutumia vifaa hivyo ipasavyo, kutunza mazingira yanayowazunguka na kuendeleza utamaduni wa kuweka taka katika maeneo maalumu.
Kupitia mipango yake ya CSR, Meridianbet inaendelea kuonesha dhamira yake ya kuwa sehemu ya jamii na kuchangia maendeleo endelevu kwa kuunga mkono juhudi zinazolenga kuboresha ustawi wa wananchi.
