Ligi Kuu ya Hispania (LaLiga) itaendelea leo Jumamosi kwa mchezo kati ya Barcelona na Deportivo Alavés utakaopigwa katika dimba la Spotify Camp Nou, jijini Barcelona. Mchezo huo utaanza saa 23:00 usiku, huku Barcelona wakilenga kupata pointi tatu muhimu ili kuendelea kujiimarisha kileleni mwa ligi hiyo.
Unautazama mchezo, lakini je, umeshachagua upande wako? Mchezo huu unapatikana Meridianbet pamoja na machaguo mbalimbali ya odds kubwa. Jisajili leo, chunguza machaguo na furahia msisimko waushindi!
Barcelona wataingia kwenye mchezo huo wakitaka kurejea kwenye ushindi baada ya kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid katika El Clásico iliyopita. Matokeo hayo yalikatisha mwenendo wao mzuri wa ushindi katika LaLiga, hivyo kocha Hansi Flick anahitaji kuona kikosi chake kikijibu kwa kupata ushindi na kuendelea kupambana kulinda nafasi yao kileleni mwa msimamo.
Kwa upande wa Deportivo Alavés, timu hiyo itasafiri kwenda Barcelona ikiwa na matumaini ya kupata matokeo mazuri licha ya kukabiliwa na changamoto ya kutokuwa na mwendelezo wa ushindi. Katika mchezo wao uliopita, Alavés walitoka sare ya bao 1-1 dhidi ya Málaga, matokeo yanayowaacha wakihitaji kuboresha umaliziaji wa mashambulizi yao ili kuwa na nafasi ya kuisumbua Barcelona ugenini.
Macho yataelekezwa kwa nyota wa Barcelona, akiwemo Lamine Yamal, ambaye uwezo wake wa kupenya upande wa kulia na kutengeneza nafasi unaweza kuwa silaha muhimu kwa wenyeji.
Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema. Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.
Hata hivyo, Barcelona wanapaswa kuwa makini katika safu ya ulinzi, hasa wanapopandisha wachezaji wengi kushambulia. Alavés wanaweza kutumia nafasi hizo kufanya mashambulizi ya kushtukiza kupitia washambuliaji wao, akiwemo
Barcelona wanaonekana kuwa na nafasi nzuri kutokana na kucheza nyumbani na umuhimu wa matokeo katika mbio za ubingwa. Hata hivyo, Alavés hawapaswi kubezwa, kwani nidhamu ya ulinzi na matumizi mazuri ya nafasi vinaweza kuwapa nafasi ya kupata matokeo. Ushindi utakuwa muhimu kwa Barcelona kurejesha hali ya kujiamini, wakati Alavés watakuwa wakisaka pointi zitakazowasaidia kuendelea kupanda katika msimamo wa LaLiga.