Kocha Mkuu Chelsea kumjengea hali ya kujiamini Mike Penders

Xabi Alonso, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa mlinda mlango Mike Penders mwenye mika 21 atakuwa langoni mchezo dhidi ya Liverpool. Mike alikuwa langoni ubao uliposoma Chelsea 0-2 Tottenham Hotspurs. Mike alijifunga dakika ya 77 na bao la pili likafungwa na Mathys Tel dakika ya 87.

Mike alikwama kuokoa kona ya Spurs, Uwanja wa Stamford Bridge pigo lake katika kuokoa lilipeleka mpira kwenye nyavu zake na dakika 10 mbele Tel akafunga bao la pili.Kipa huyo amechukua mikoba ya Emiliano Martinez ambaye alipata maumivu kwenye mchezo vs Everton.

Alonso anatarajia kumpa nafasi kikosi cha kwanza Jumatano vs Liverpool, Uwanja wa Anfield. Pambano hili linavutia kwa kiwa kocha anakutana na timu yake ya zamani katika mchezo wa Carabao Cup,raundi ya 4.

Alonso amethibitisha kwamba Penders ataanza vs Liverpool ugenini.Kocha huyo amesema anaimani na kipa huyo kutokana na uwezo alionao.Kwenye mchezo uliopita Cole Palmer alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 80.

“Ni sehemu ya mchezo kwa yaliyotokea, tunahitaji kufanyia kazi makosa.Tunaongeza hali ya kujiamini kwa Mike na atakuwa langoni kwenye mchezo dhidi ya Liverpool.Tunashinda na tunapoteza pamoja na ni sehemu ya kazi kushughulikia makosa. Mimi mwenyewe na kila mmoja,” amesema.

…

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.

Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.

Kuvipata mtandaoni bofya hapa Buy Book: Msichana wa Maisha Yangu by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar.

Buy Ganzi ya Maumivu Book by Lunyamadzo Mlyuka on Selar | selar

Moyo Wangu Unavuja Damu: https://selar.com/7901h4koj4