Aston Villa 2-1 Manchester City Emery Aandika Historia

Aston Villa imeifunga Manchester City mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi Kuu England.

Matokeo hayo yatakuwa ya furaha kubwa kwa kocha Unai Emery, ambaye katika kipindi cha miaka minne tangu ajiunge na Aston Villa, ameiongoza timu hiyo kupata ushindi katika mechi nne mfululizo za nyumbani dhidi ya Manchester City.

Ushindi huo pia ni wa kwanza kwa Aston Villa nyumbani katika msimu huu.