Simba SC 6-1 Mashujaa FC ni matokeo rasmi mchezo wa NBC Premier uliochezwa Uwanja wa Uhuru Oktoba 13,2026. Mabao ya Simba SC yamefungwa na Libase Gueye dakika ya 16 kwa asisti Neo Maema, Ellie Mpanzu dakika ya 33 na 58 Oura dakika ya 52, Abraham Morice dakika ya 61 na Ismail dakika ya 68.
Ellie Mpanzu amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo kutokana na kiwango ambacho alionyesha kwenye mchezo wa leo ikiwa ni mara ya pili mfululizo alianza Oktoba 10,2026 dhidi ya Yanga SC.
Mashujaa FC walipachika bao dakika ya 63 kupitia kwa Seleman Bwenzi.Huu ni ushindi wa kwanza mkubwa ndani ya NBC Premier League 2026/27 kwa Simba SC.
Simba SC inafikisha mchezo wa 8 bila kufungwa chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker inaongoza ligi ikiwa na pointi 24 inafuatiwa na Yanga SC iliyo nafasi ya pili na pointi 18 baada ya mechi 7.
Huu ni ushindi mkubwa kwa Simba SC na yamefungwa jumla ya mabao 7 katika dakika 90 za kazi.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.