ELLIE Mpanzu, nyota wa Simba SC mfungaji wa bao la ushindi dakika ya 71 amefichua kile alichoandika Uwanja wa Uhuru wakati akishangalia.
Oktoba 10,2026 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba SC 2-1 Yanga SC, bao la Peter Shalulile dakika ya 5 lilidumu mpaka dakika ya 68.
Simba SC ilifungua ukurasa wa mabao kupitia kwa Neo Maema dakika ya 68 akitumia pasi ya Libase Gueye. Bao la ushindi limefungwa na Ellie Mpanzu dakika ya 71 akitumia pasi ya Kaletso Makgalwa.
Mnyama alipindua meza kipindi cha pili kwa kuongeza mashambulizi kwa Yanga SC ambao walisuka ukuta imara katika dakika 45 za mwanzo.
Chini ya Kocha Mkuu, Steve Barker wachezaji wa Simba SC wametibua rekodi ya Yanga SC kutofungwa ndani ya ligi msimu wa 2026/27 baada yakucheza mechi 6 mfululizo na kupata ushindi asilimia 100.
Nyota Ellie Mpanzu ambaye alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo mara baada ya dakika 90 za kazi kukamilika mzunguko wa kwanza wakati wa kushangilia alionekana akiandika maneno chini.
Kwa mujibu wa Simba SC wamebainisha kuwa aliandika “Thank You God” ikiwa inamaanisha Asante Mungu.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.