Baada ya kimya kirefu cha takribani siku 21, hatimaye ligi zinarudi kwa kishindo huku timu mbalimbali zikijiandaa kushuka dimbani kusaka pointi tatu za ushindi. Je nani kushinda leo?
Leo hii kule Uingereza kutakuwa na mechi kubwa ambayo itavuta hisia za mashabiki wengi wa soka Duniani ambapo katika dimba la Anfield Liverpool atakuwa nyumbani kumenyana dhidi ya Manchester City ambapo kila timu inahitaji kupata ushindi siku ya leo.
Kwenye msimamo wa ligi, Liver mpaka sasa ana pointi 9, huku City wao wakiwa na pointi 15 na ndio vinara wa ligi kuu hadi sasa wakiwa wameshinda mechi zote 5 walizocheza hadi sasa, hivyo hadi sasa tofauti yao ni pointi 6.

Hii ni mechi ambayo inazikutanisha timu mbili ambazo zina makocha wapya, yaani kwa upande wa Liver Iraola ambaye alichukua mikoba ya Arne Slot, huku City wao mpaka sasa wapo chini ya Enzo Maresca ambaye ndio ameaminiwa kuchukua mikoba ya Pep Guardiola na mpaka sasa ameshinda mechi zote.
Kila timu ina wachezaji wengi tena wakubwa ambao wana uwezo wa kubadili matokeo yoyote, wakiwemo kina Erling Haaland, Enzo, Doku, na wengine, huku kwa Majogoo kuna Barcola, Wirtz, Gakpo na wengine wengi.
Mechi hizi zinapatikana kule Meridianbet, lakini pia kwa taarifa zote na misimamo ya ligi mbalimbali unaipata huko.
Takwimu zinaonesha kuwa msimu uliopita, kwenye mechi mbili za ligi ambazo wamekutana City ameibuka mshindi, hivyo hii ni nafasi ya vijana wa Iraola kulipa kisasi. Je watweza?.
Pia kule Italia, SERIE A itaendelea kwa mechi nyingine, lakini mechi ya kibabe ni hii ya Como 1907 dhidi ya AS Roma ambao mpaka sasa wapo kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi wakiwa na pointi 13.
Wakati kwa upande wa Como ya Fabregas mpaka sasa wao wapo nafasi ya 8 wakiwa na pointi 10 ambapo tofauti ya pointi kati yao ni 3 hadi sasa, huu ni ushindi ambapo timu zote mbili unauhitaji kwa hali na mali.
Como licha ya kupotea mechi yake iliyopita, ina faidi ya kucheza mechi hii nyumbani hivyo hautakuwa ni mchezo rahisi wa wageni wao kutokana na kuwa pia wana wachezaji wazuri kwenye eneo la ushambiliaji kama vile Nico Paz.
Kwa upande wa Roma, mchezaji wao Mallen ametoka kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mwezi kutokana na kiwango bora ambacho amekionesha mwezi September hivyo hii ni nafasi nzuri ya kuonesha hivyo pia kwenye mechi muhimu kama hizi.
Msimu uliopita kila timu ilishinda mechi ya nyumbani kwake. Je leo hii nani ataondoka na ushindi kwenye mechi hii ya mkondo wa kwanza?