Taifa Stars Kutupa Karata Yake Ya Kwanza Kuwania Kufuzu Afcon 2027 leo

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars inatarajiwa kushuka dimbani kesho siku ya ijumaa majira ya saa 10 kamili jioni katika uwanja wa New Amaan Complex uliopo Zanzibar,kupambana na Geinea Bissau.

Mchezo huo utakaopigwa huko Zanzibar ni mchezo wa Kwanza Kwa timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars na unaangaliwa kama mojawapo ya njia ya maandalizi kuelekea AFCON 2027

kikosi hicho tayari kimewasili visiwani Zanzibar tayari Kwa mchezo huo mgumu dhidi ya Guinea Bissau.

Ikumbukwe kuwa Taifa Stars imetoka kushiriki michuano ya AFCON ambayo ilifanyikia nchini Morroco na ikaishia katika hatua ya mtoano, hatua ambayo iliicheza Kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa Kwa Taifa hilo.

AFCON 2027 itakauofanyikia Tanzania Kenya na Uganda inatajwa kuwa ni moja ya AFCON ya kihistoria Kwa nchi hizo hivyo Taifa Stars inajipanga kufanya makubwa katika michuano ijayo.
Na.Clever Alphonce