Real Betis, Getafe kukutana kwenye vita ya pointi LaLiga

Real Betis itakuwa mwenyeji wa Getafe katika mchezo wa ligi kuu ya uhispania Laliga utakaochezwa leo Alhamisi, Septemba 17, 2026, kwenye Uwanja wa Estadio La Cartuja mjini Sevilla. Mchezo huo wa raundi ya sita unatarajiwa kuanza saa 20:00 usiku.

Betis inaingia kwenye mchezo huo ikiwa na matumaini ya kuendeleza kiwango kizuri kilichoanza kuonekana katika mechi zake za hivi karibuni. Kikosi cha Manuel Pellegrini kimekuwa kikionyesha ushindani mkubwa, huku ushindi dhidi ya Real Madrid ukiwa miongoni mwa matokeo yaliyoongeza kujiamini kwa timu hiyo na kushikilia nafasi ya saba na alama tisa.

Kwa upande wa Getafe, timu hiyo itakuwa na kazi ya kuhakikisha inapata matokeo mazuri ugenini baada ya kupata sare ya 1-1 dhidi ya Deportivo La Coruña katika mchezo wake uliopita wa ligi.

Getafe pia ina kumbukumbu nzuri dhidi ya Betis, kwani iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mchezo wao wa mwisho kwenye ligi mwezi Machi. Kwasasa Getafe wapo nafasi ya 14 kwenye msimamo huku wakifanikiwa kukusanya alama tano baada ya kucheza michezo mitano.

Meridianbet inasema kuna michezo kama Keno, Aviator, Poker, Roulette, Wild Icy Fruits, Super Heli. Ingia katika kasino ya mtandaoni ya Meridianbet na ujiokotee mkwanja mapema.  Jiunge sasa au Tembelea tovuti ya meridianbet.co.tz au piga *149*10# kisha uanze safari yako ya ushindi.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kutokana na tofauti ya mitindo ya timu hizo. Betis inaweza kutegemea ubora wa wachezaji wake kama Anthony na Isco wakati wa kushambulia na faida ya kucheza kwenye uwanja wake wa nyumbani, wakati huohuo Getafe itahitaji kuwa makini katika ulinzi na kutumia nafasi zitakazopatikana kwenye mashambulizi ya kushtukiza.

Kwa ujumla, macho yatakuwa kwa Betis kuona kama itaweza kutumia uwanja wa nyumbani kupata pointi tatu ambazo zitawasogeza hadi nafasi ya tano au ya nne, huku Getafe ikisaka matokeo yatakayoiweka katika nafasi nzuri mapema msimu huu ili kujiepusha na kushuka daraja mwishoni mwa msimu.