MTAJIRI wa Dar, Azam FC wameanza na ushindi kwenye mchezo wa nyumbani msimu wa 2026/27 baada ya kuanza na sare ugenini dhidi ya Polisi Tanzania.
Baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex Agosti 20,2026 ulisoma Azam FC 2-1 TRA United.
Ni Idd Suleman alianza kufunga dakika ya 8 na Abdul Suleiman alipachika bao la pili kwenye mchezo huo dakika ya 33.
Bao pekee la TRA United lilifungwa na Ousmane Kamisoko dakika ya 45.Matajiri wanafikisha pointi 4 nafasi ya 5 kwenye msimamo, TRA United nafasi ya 11.
Mlinda mlango wa Azam FC, Aishi Manula alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 75 na mwamuzi Ahmed Arajiga mara baada ya kumchezea faulo mchezaji wa TRA United Kamisoko ambaye alikuwa kwenye nafasi yakufunga bao kipindi cha pili.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.