Singida Black Stars vs Simba SC NBC Premier League ni mchezo unaofuata kwa wababe hawa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Airtel, Singida.
Huu unakuwa ni mchezo wa tatu kwa wababe hawa kushuka uwanjani kusaka pointi 3 muhimu msimu mpya 2026/27 ambao umeanza kwa kasi.
Simba SC itaingia uwanjani bila huduma ya Duchu ambaye alionyeshwa kadi nyekundu mchezo dhidi ya Kagera Sugar na Ibraheem Jaabar ambaye alionyeshwa kadi nyekundu mchezo dhidi ya Pamba Jiji FC.
Katika mechi mbili wachezaji wawili wa Simba SC wameonyeshwa kadi nyekundu za moja kwa moja kutokana na kucheza faulo kwa wachezaji wa timu pinzani.
Steve Barker, Kocha Mkuu wa Simba SC amesema kuwa wanafanyia kazi makosa yaliyopita ili kuwa imara kwa mchezo ujao dhidi ya Singida Black Stars.
Uongozi wa Singida Black Stars kupitia kwa Ofisa Habari, Hussen Masanza wamebainisha kuwa watapambana kupata pointi 3 muhimu baada ya dakika 90.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, Moyo Wangu Unavuja Damu na Msichana wa Maisha Yangu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Msichana wa Maisha Yangu ni simulizi mpya ambayo inazungumzia nguvu ya ahadi na mabadiliko ya teknolojia ikiwemo matumizi ya AI. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.