BENCHI la ufundi la Yanga SC chini ya Kocha Mkuu, Manqoba Mngqithi limefanya ‘umafia’ kwa kunasa faili zima la wapinzani wao Coastal Union kabla ya kuwakabili leo Agosti 20,2026 Uwanja wa KMC Complex.Huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa mabingwa watetezi wa ligi kushuka uwanjani, wamekusanya pointi 3 baada ya ushindi dhidi ya Namungo FC wapo nafasi ya 3 kwenye msimamo vinara ni watani zao wa jadi Simba SC wenye pointi 6 baada yakucheza mechi 2.
Manqoba ambaye ni mchora ramani mkuu kwenye mbinu za ufundi amesema kuwa aliwatazama wachezaji wa timu hiyo kwa umakini katika mchezo uliopita dhidi ya Mashujaa FC walipopoteza kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Kocha huyo amesema “Coastal Union ni timu ambayo tunapaswa kuwa nayo makini sana. Nimemtazama kipa wao (Chuma Ramadhan), mabeki wao wa kati si wabaya na viungo wao wa kati, Godfrey na Ally, ambao walicheza vizuri katika mchezo uliopita.
“Wapinzani wetu tunawaheshimu kutokana na kuonyesha ushindani mkubwa. Wako vizuri kwenye mipira ya juu kwa sababu washambuliaji wao ni warefu. Tunajua tunakwenda kucheza na timu gani, na tunajua ubora walio nao,” alisema Manqoba.
Lunyamadzo Mlyuka