Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) kupitia bodi ya sheria za mchezo (IFAB) limetangaza mabadiliko mapya ya sheria tisa yatakayotumika kuelekea na wakati wa Kombe la Dunia 2026, hatua inayolenga kuongeza kasi ya mchezo, kupunguza upotevu wa muda na kuboresha matumizi ya VAR.
Kombe la Dunia 2026 linatarajiwa kuanza Juni 11 huko Mexico City, na mabadiliko haya yanatajwa kuwa miongoni mwa makubwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni.
1. VAR kuchunguza makosa kabla ya kona na free-kick
VAR sasa itaruhusiwa kuchunguza makosa yanayotokea kabla ya mpira kupigwa kwenye kona au free-kick, hususan kushikana au kuvutana ndani ya boksi. Tukio likibainika, adhabu inaweza kuwa ni kurudiwa kwa mpira.
2. Sekunde 5 kwa throw-in
Wachezaji watatakiwa kufanya throw-in ndani ya sekunde tano. Kushindwa kufanya hivyo kutapelekea mpira kupewa timu pinzani.
3. Sheria mpya ya goal-kick
Goal-kick lazima ipigwe haraka zaidi. Endapo kutakuwa na ucheleweshaji mkubwa, adhabu inaweza kuwa kona kwa timu pinzani.
4. Kadi nyekundu kwa mawasiliano ya “aggressive”
Mchezaji atakayezungumza na mpinzani kwa njia ya kuonyesha uchokozi au kumfokea akiwa amefunika mdomo anaweza kupewa kadi nyekundu.
5. Kuondoka uwanjani kwa hasira ni adhabu
Mchezaji au kocha anayetoa ishara ya kuondoka uwanjani kupinga uamuzi wa refa atapewa kadi nyekundu moja kwa moja.
6. Wachezaji kutoka uwanjani ndani ya sekunde 10
Baada ya kubadilishwa, mchezaji anatakiwa kutoka haraka ndani ya sekunde 10. Akikaidi, mchezaji mpya hataruhusiwa kuingia mara moja.
7. Adhabu ya kuchelewa kurudi uwanjani
Mchezaji anayetoka kwa ajili ya matibabu atalazimika kusubiri dakika moja kabla ya kurudi uwanjani, isipokuwa kwa majeraha maalum kama ya kipa au matukio ya penalty.
8. VAR kupanuliwa mamlaka
VAR sasa inaweza kuingilia katika:
- Kadi za pili za njano
- Utambulisho sahihi wa wachezaji
- Maamuzi ya kona yaliyo na utata
9. Mapumziko ya maji ya lazima
Kila mchezo utakuwa na mapumziko ya dakika tatu ya kunywa maji katikati ya kila kipindi ili kulinda afya ya wachezaji.