MECHI za leo Mei 25, 2026 ni moto wa kuotea mbali na zinapigwa Uwanja wa KMC Complex kwa wababe kusaka pointi tatu muhimu ndani ya dakika 90.
Yanga SC hawa ni mabingwa watetezi wa ligi watamenyana na Namungo FC kwenye mchezo wa mzunguko wa pili.
Wababe hawa wanatarajiwa kukutana saa 12:30 kusaka pointi 3 muhimu ndani ya uwanja.
Wakusanya mapato ya Kinondoni, KMC FC watashuka uwanjani kukabiliana na Azam FC ni saa 3:00 usiku.
Mabingwa watetezi wapo nafasi ya pili na pointi 57 baada ya mechi 24 wanakutana na Namungo FC nafasi ya 13 pointi 25, KMC FC ina pointi 9 ipo kwenye mstari wakushuka daraja huku Azam FC ikiwa nafasi ya 3 na pointi 49.
…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.