Dodoma Jiji FC vs Yanga SC kinawaka kesho Mei 13, 2026 Uwanja wa Airtel Singida ambapo kila timu inapambania pointi tatu muhimu.
Yanga SC ni timu pekee ambayo haijapoteza mchezo ndani ya ligi namba nne kwa ubora inakutana na Dodoma Jiji FC ambayo imepoteza jumla ya mechi 7.
Mlinda mlango wa Dodoma Jiji FC, Hussen Masalanga ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo huo na wanawaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi.
“Kwa niaba ya Wachezaji wenzangu tumejiandaa vizuri na mchezo wa kesho na kila mmoja wetu anajua umuhimu wake. Kwa sasa lengo letu ni kuhakikisha tunashinda kila mchezo.
Mashabiki wetu wamekuwa msaada mkubwa sana msimu mzima. Tunahitaji sauti yao, nguvu yao na sapoti yao katika kila mchezo. Tunawaomba wajitokeze kwa wingi kesho ili kutupa nguvu ya kupambana na kupata ushindi.”