Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, leo Mei 4, 2026 amewasili katika viwanja vya Bunge la Tanzania jijini Dodoma akiwa pamoja na gwiji wa soka wa Ivory Coast, Didier Drogba.
Drogba, ambaye anajulikana sana kwa mafanikio yake akiwa mshambuliaji wa klabu ya Chelsea F.C., alihudhuria tukio hilo maalum ambapo Makonda alikuwa akiwasilisha Hotuba ya Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2026/2027.
Uwepo wa Drogba unaashiria umuhimu wa michezo kimataifa na mchango wake katika diplomasia ya kijamii na maendeleo ya sekta ya michezo nchini.
