Kagoma, Kibabage kuikosa Kariakoo Dabi?

NYOTA wa Simba SC Nikson Kibabage, Anicent Oura na Yusuph Kagoma uwezekano wa kuikosa Kariakoo Dabi kesho ni mdogo kulingana na maendeleao yao kuzidi kuwa imara.

Awali wachezaji hao walileta mshtuko kutokana na maumivu ambayo walipata kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi, Muungano Cup 2026 dhidi ya Yanga SC, Uwanja wa New Amaan Complex.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba SC amesema kuwa wachezaji hao wanaendelea vizuri hivyo ni maombi kwa Mungu wazidi kuwa imara.

“Ikumbukwe baadhi ya wachezaji wetu muhimu walipata majeraha katika mchezo wa Fainali ya Muungano Cup, dhidi ya Yanga SC na kuleta hofu kuelekea mchezo huu.

“Baadhi ya wachezaji hao ni Anicet Oura, Nickson Kibabage na Yusuph Kagoma. Napenda kuwajulisha kwamba wachezaji hao wote ambao walitolewa katika mchezo wa fainali ya Kombe la Muungano kwa kuumia, wako tayari kwa mchezo wa Jumapili. Ninapozungumza hapa wachezaji wapo vizuri kabisa, Tunamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kulinda hali zao.”

Saa 12:00 mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Meja Isahmuyo kwa wababe hawa wawili kusaka pointi tatu muhimu.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.