IDD Seleman Nado nyota wa Azam FC amenadika rekodi yake kwenye mchezo wa kiporo dhidi ya Singid Black Stars kwa kukoleza moto uliofanya kiporo kisichache.
Kiungo huyo alihusika kwenye magoli yote mawili yaliyofungwa na timu hiyo ambayo ipo nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi msimu wa 2025/26 baada ya kucheza jumla ya mechi 16 ikiwa na pointi 32.
Simba SC nafasi ya pili ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 15 leo inatarajiwa kushuka Uwanja wa Meja Jenerali Isahmuyo kukabiliana na Coastal Union ya Tanga, saa 1:00 usiku.
Nado alitoa pasi ya kwanza kwa Lusajo dakika ya 50 ikiwa zimepita dakika 5 kipindi cha pili kuanza kwani dakika 45 za mwanzo ngoma ilikuwa 0-0.
Dakika 13 mbele akatoa pasi nyingine kwa Feisal Salum dakika ya 63 ambaye alifunga goli la ushindi kwenye mchezo huo.
Goli la Singida Black Stars lilifungwa na Ayoub Lyanga dakika ya 70 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na kufanya ubao wa Uwanja wa Airtel kusoma Singida Black Stars 1-2 Azam FC.
Nado alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo mara baada ya dakika 90 kutamatika.
***
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu. Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.
Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.