Timu ya Taifa ya DR Congo National Football Team, maarufu kama The Leopards, imeandika historia kwa kufuzu FIFA World Cup 2026 baada ya ushindi mwembamba wa 1-0 dhidi ya Jamaica National Football Team katika mchezo wa mchujo uliochezwa alfajiri ya leo nchini Mexico.
Bao pekee la ushindi lilifungwa dakika ya 100 na Axel Tuanzebe, katika muda wa ziada, likihakikisha ushindi muhimu uliovunja ukame wa zaidi ya miaka 52 kwa taifa hilo kurejea kwenye fainali za Kombe la Dunia.
Hii ni mara ya pili kwa DR Congo kufuzu michuano hiyo mikubwa duniani, ikiwa ni kurejea kwa kishindo tangu waliposhiriki kwa mara ya kwanza mwaka 1974.
Katika upangaji wa makundi, DR Congo imepangwa Kundi I ambapo itakutana na mataifa yenye ushindani mkubwa ambayo ni Portugal National Football Team, Uzbekistan National Football Team na Colombia National Football Team.
Kwa kufuzu huku, DR Congo inakuwa taifa la 10 kuiwakilisha Afrika kwenye michuano ya 2026, ikiungana na Algeria National Football Team, Cape Verde National Football Team, Egypt National Football Team, Ghana National Football Team, Ivory Coast National Football Team, Morocco National Football Team, Senegal National Football Team, South Africa National Football Team na Tunisia National Football Team.
Matokeo ya Mwisho:
DR Congo 🇨🇩 1-0 🇯🇲 Jamaica
⚽ Dakika ya 100 – Tuanzebe
Ushindi huu unaashiria mwanzo mpya kwa soka la DR Congo, likiwa na matumaini makubwa kuelekea michuano ya mwaka 2026.