Italia Yatolewa kwa Aibu, Bosnia Yatinga World Cup 2026

Timu ya Taifa ya Italy National Football Team imeendelea kukumbwa na jinamizi la kukosa FIFA World Cup 2026 baada ya kushindwa kufuzu kwa mara ya tatu mfululizo (2018, 2022 na 2026).

Italia imeondoshwa kwenye mchujo wa mwisho kufuatia kipigo cha penalti 4-1 dhidi ya Bosnia and Herzegovina National Football Team, baada ya sare ya 1-1 ndani ya dakika 90 za kawaida.

Katika mchezo huo, Alessandro Bastoni aliifungia Italia dakika ya 15 kabla ya kulimwa kadi nyekundu dakika ya 41, hali iliyobadili mwelekeo wa mchezo. Bosnia ilisawazisha kupitia Haris Tabaković dakika ya 79 na kulazimisha mchezo kwenda penalti, ambapo waliibuka washindi kwa 4-1.

Matokeo:
Bosnia 🇧🇦 1-1 🇮🇹 Italy (Pen: 4-1)
⚽ 15’ Bastoni
🟥 41’ Bastoni
⚽ 79’ Tabaković

Kwa upande mwingine, Czech Republic National Football Team imefanikiwa kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Dunia baada ya ushindi wa penalti 3-1 dhidi ya Denmark National Football Team.

Mchezo huo ulikuwa mkali na kumalizika kwa sare ya 1-1 ndani ya dakika 90, kabla ya kuongezwa dakika za ziada na kufikia 2-2, kisha Czech Republic kuibuka na ushindi kwenye mikwaju ya penalti.

Matokeo:
FT: Czech Republic 🇨🇿 1-1 🇩🇰 Denmark (ET: 2-2) (Pen: 3-1)

Matokeo haya yanaifanya Bosnia & Herzegovina na Czech Republic kujiunga na mataifa mengine yaliyofuzu, huku Italia ikiendelea kuwa nje ya ramani ya Kombe la Dunia kwa kipindi cha zaidi ya muongo mmoja sasa.