Bacca amuombea Job kurejea uwanjani haraka

BEKI wa Yanga SC, Ibrahim Bacca ameweka wazi kuwa anamuombea beki Dickson Job ili arejee uwanjani haraka kutokana na kuwa nje kwa muda mrefu.

Job alipata maumivu kwenye mchezo wa NBC Premier League dhidi ya Simba SC, uliochezwa Uwanja wa New Amaan Complex, taarifa za awali zimeeleza kuwa huenda atakuwa nje ya uwanja kwa msimu mzima akipambania kurejea katika ubora.

Bacca amesema: “Mimi kwa upande wangu namiss uwepo wake na pia tunamiss uwepo wake, tunamuombea kwa Mweneyezi Mungu apone haraka hata kwa msimu huu aweze kurejea kwa kuwa kwa Mwenyezi Mungu hakuna kinachoshindikana.

“Sisi tunapambana kwa ajili yake na hata Clement Mzize pia tunamoembea apone haraka kwa kuwa sisi tunaendelea kupambana kwa ajili ya kuona timu inapata matokeo mazuri uwanjani,”.

Yanga SC ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 38 baada ya mechi 16. Hawajapoteza mchezo mpaka sasa ndani ya ligi na mchezo wao ujao ni dhidi ya Tanzania Prisons unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex, Aprili 4, 2026.

***

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo na Moyo Wangu Unavuja Damu.  Kuvipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371.

Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Msichana wa Maisha Yangu, jiandae kuipata.